Saturday, May 17, 2014

ALIYEVUJISHA VIDEO YA JAY Z AKIPIGWA NA SHEMEJI YAKE ATIMULIWA KAZI…!SOMA ZAIDI

JAMAA aliyevujisha video ikionyesha staa Jay Z akipigwa na shemeji yake Solange ametimuliwa kazi.
Hoteli ya New York Standard  imeamua kusitisha mkataba wa jamaa huyo mara moja baada ya kuvunja sheria za usalama za hoteli hiyo kwa kuvujisha tukio nyeti kama hilo.
JAYZ
Solange (mbele kulia) baada ya kumpa kichapo shemeji yake Jay Z (wa tatu kushoto)
Jamaa huyo anadaiwa kuwauzia TMZ kipande hicho cha video kwa dola 250,000 sawa na shilingi 412,500,000 za Tanzania.
HAPO CHINI NI VIDEO YA JAY Z ALIPOPEWA KICHAPO NA SOLANGE