Kwao ni kitu cha kawaida na hawaoni aibu kuanika maungo yao katika mitandao ya jamii na hawaoni aibu hata kushiriki mapenzi ya jinsia moja,tumesikia ushoga ndani ya bongo movie,tumesikia usagaji ndani ya bongo movie na sasa ni picha za uchi ndani ya bongo movie,badala ya kukaa na kutafuta connection za kufanya kazi kimataifa wao wanatafuta tension na umaarufu kwa kufanya mambo yaliyo kinyume na jamii. Viongozi wao inaonekana kulemewa kama si kushindwa kukemea na kurudisha heshima katika kikundi hicho cha wasanii na kila mmoja kujiamulia na kufanya mambo ya aibu kwa kadri ya uwezo wake.