Mtu mmoja ambaye alikuwa akishiriki vitendo vya wizi alijikuta akimpa Yesu maisha yake hapo jana mara baada ya kukimbilia kanisa la The Oasis Healing Ministries lililopo nyuma ya jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam, mara baada ya mwizi huyo kukimbilia kanisani hapo akisalimisha maisha yake baada ya kuiba alikotoka.
Mwizi huyo ambaye hata hivyo GK haikupata jina lake, mara baada ya kukimbilia kanisani hapo, aliweza kuhubiriwa neno la Mungu ambalo alilipokea na kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kuahidi kuendelea kumshika na kumkiri Yesu, hata kokote atakapopelekwa na jeshi la polisi ambao walifika kanisani hapo kumchukua mwizi huyo.
Tukio la mwizi huyo kumpokea Yesu lilipokelewa kwa shangwe na waumini wa kanisa hilo ambao walishindwa kuzuia furaha hiyo hata mwizi huyo alipopandishwa kwenye gari ya polisi, ambapo mchungaji alimuombea huku mwizi huyo akionekana mwenye utulivu.