Monday, May 26, 2014

KINARA WA KUSAFIRISHA MABINTI NA KUWAUZA HUKO INDIA HUYU HAPA, SOMA KUJUA ZAIDI

Wakifika India hunyang'anywa passport mpaka watakapomaliza kulipa $ 4000
Wengine hulazimishwa kufanya kinyume na maumbile
Gossip Court imefanikiwa kupata Chats za Whatsapp

Iko hivi, kama binti anataka kuja huku india ye yuko Tanzania anaunganishwa na Shumy halafu Shumy anatumiwa picha za mabinti sasa hapo inategemea na uzuri wa binti,maana Shumy anasafirisha mabinti wakali tu,then Shumy akiwapenda anawatumia pesa ya VISA kwa ajili ya hao mabinti ambayo ni 70,000 za kitanzania kila mmoja,halafu wakishapata Viza anakata ticket huku India then anawatumia kwa E-mail wanaprint Tanzania halafu wakifikia India wananyang'anywa passport mpaka watakapomaliza kulipa deni la $ 4000,na kazi wanayofanya ni kujiuza mitaa ya India na akimaliza kulipa deni anarudishiwa passport yake na anakua huru kuamua anarudi Tanzania au anabaki huku,asilimia kubwa wanabaki huku na wanaolewa ndoa zisizo rasmi na wanigeria,wakongo ama raia wa nchi zingine maana wahindi wao wanaoana wao kwa wao.Na kwao huko Tanzania wanajua mabinti wamekuja kutafuta kazi wengine wanadanganya wanakuja kusoma,na hata wale wanaokuja kwa nia ya kusoma pia nao wamo katika hili la kujiuza,chanzo hicho kilisema.

Chanzo chetu kiliongeza kua "Hakuna ambae yuko India hajui hiyo biashara ya mabinti kusafirishwa kuja kufanya umalaya huku na wengine hutoka bila kutumia kondomu na wengine walishawahi kupata mimba"