Akizungumza na paparazi, Mainda alisema kuanzia sasa watu wategemee mabadiliko makubwa katika maisha yake kwani ameamua kuvikacha viminihivyo anaishi katika matakwa ya dini.
“Nitafanya filamu za kumtukuza Mungu hata kama zitakuwa si za kumtukuza moja kwa moja ila zitakuwa na maadili mazuri yasiyopotosha jamii na kumuudhi Mungu, sitavaa vimini tena,’’ alisema Mainda.