Monday, May 26, 2014

Viatu vya KANUMBA vyakosa mvaaji…Wasambazaji wa Filamu walalamika Mauzo kushuka..!

Wasambazaji wa filamu wanasema hakuna mauzo tena ya filamu toka kifo cha marehemu Steven Kanumba, wanalalamika kuwa mauzo yameshuka sana hadi hata wengine kuachana na biashara hiyo na kuamua kufanya biashara nyingine zinazowalipa.
Inawezekana maneno yao yakawa sahihi au si sahihi, kutokana na hali halisi ya mfumo wa tasnia ya filamu ulivyo hasa katika idara ya mauzo, sasa kila mtu anajaribu kutafuta sehemu gani ya kuangukia ndio tunasikia wakisema kuwa toka kifo cha Kanumba hakuna mauzo ya filamu.
1
Hayati Steven Kanumba Mtayarishaji na mwigizaji Nyota Swahiliwood
Kanumba akiwa katika pozi
Kanumba akiwa katika pozi

Umati wa watu siku ya mazishi ya Kanumba
Umati wa watu siku ya mazishi ya Kanumba
Hayati Kanumba akiwa na mwigizaji wa kimataifa Ramsey Noah kutoka Nigeria
Hayati Kanumba akiwa na mwigizaji wa kimataifa Ramsey Noah kutoka Nigeria

Kanumba akiwa nchini Ghana
Enzi za uhai wake Kanumba the Great
Ni kweli hakuna ubishi kuwa Kanumba alikuwa na mvuto wa kipekee katika tasnia ya filamu Bongo lakini hatuna mbadala wake? Ambaye anaweza kuvaa viatu vyake na kuifanya tasnia ya filamu ifanye vizuri kama awali! Inashangaza sana kwani inaonekana kuwa msanii huyo alitengenezwa na kuwa alivyokuwa.
Hivi karibuni ilitoka tathamini kuwa kuwa filamu zinazoongoza kwa mauzo kwa muda mrefu ni tano tu, ambazo ni 1. Furaha iko wapo 20%, 2. Kigodoro, 3. Mwali wa Kizaramo, 4.Bado Natafuta, 5. Ndoa yangu ambayo ni kazi ya marehemu Kanumba na huku kazi za msanii ambaye hayupo Duniani zikiendelea kufanya vizuri sokoni.
Ukimtoa Kanumba hapo utagundua filamu ambazo zinaonekana kufanya vizuri si zilizochezwa na wale wasanii nyota ambao ndio wamezoeleka kuwa ni vinara vya kuzalisha filamu Swahiliwood, bali ni kazi zilizofanywa na wasanii chipukizi au wasiopewa nafasi katika tasnia ya filamu Bongo.
Hivyo inawezekana ikawa tatizo si kutoweka kwa Kanumba ndio sababu ya kushuka kwa soko la filamu Swahiliwood, nafikiri una kitu cha kujifunza hapa kwa wasambazaji wa filamu zetu badala ya kuuza au kusambaza sinema kwa mazoea wabadilishe mfumo wa usambazaji.
Pengine ushindani wa wasanii wawili yaani marehemu Kanumba na Ray vilichochea mbio za tasnia ya filamu na wao kutumika kuwa ni vinara wa tasnia hiyo, kwani hadi sasa toka kifo cha Kanumba hata muonekano wa Ray umepotea kabisa haonekani.
Kwa sasa unaweza kumsikia Ray akiongelewa kuhusu mahusiano yake na msanii mwenzake Ray na si kuhusu kazi zake anazotengeneza tofauti na hapo awali, ambapo wasanii watambulika kwa kazi zao, lakini kwa sasa wasanii wetu wanabainishwa kwa kashifa zinazowakabili kama watu nyota si kwa kazi zao.
Lakini kuna tatizo lingine ambalo linaikumba tasnia yetu ya filamu Bongo ni ile hali ya baadhi ya wasanii kukosa ubunifu na kutafuta mbinu au ubunifu ambao utawatambulisha wao zaidi ya kutumia muda mwingine kuweka nywele zao wave ili wafanane na marehemu Kanumba na si kutafuta siri ya mafanikio yake.
Kuna vitu vingi ambavyo marehemu aliweza kuvifanya na vikamtambulisha yeye kama ni moja kati ya wasanii maarufu Tanzania kutokea katika tasnia ya filamu Bongo, lakini leo hii tunampataje mtu kama yeye jibu ni hakuna, tofauti yake na waliobaki ni kwamba wameridhika na umaarufu wa ndani si kutafuta njia za kimataifa.
Tumeona juhudi za baadhi ya wasanii wa filamu ambao wameweza kujaribu kufuata nyayo zake kwa mbali sana, mfano ni kama Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ameweza kuingia mikataba na baadhi ya makampuni kama vile Airtel na Steps Solar pia akiwa mrithi wa nafasi ya marehemu Kanumba kama Balozi wa Oxfarm.
Lakini kuna kitu kimekosekana kwa JB pamoja na kuwa ni balozi wa makapuni kadhaa lakini bado hakuna muonekano mkubwa kwake na kuweza kusikika kama Kanumba hatujui sababu ni nini? Kwani yale yaliyofanywa na Kanumba ndio ambayo anayafanya JB.
Jb amekuwa akilaumiwa kwa tabia yake ya kujisikia na kushindwa kutoa ushirikiano kwa baadhi ya waandishi wa habari pale wanapotaka kuongea naye zaidi ya wale anaoamini ni rafiki zake ambao anaweza kuwatumia kwa matangazo na kumsifia sana bila kumkosoa hata kama atakuwa amekosea kama mwanajamii.
Hivyo tunategemea kuendelea kuliona pengo hilo ambalo ni wazi limeonekana kwa kupitia kwa wauzaji wa filamu ambao ni wadau wakubwa katika tasnia ya filamu Swahiliwood, tunahitaji mabadiliko makubwa hasa kwa upande wa mauzo kwani soko ni baya sana kwa sasa na hakuna juhudi za makusudi katika kunasuka.
Wasanii na wadau wa tasnia ya filamu tuna kazi kubwa sana katika kuliweka sawa hili suala la maslahi ni tatizo kubwa kama halitashughulikiwa tutakuwa mashuhuda tasnia hiyo ikipotea kama vile muziki wa Bongofleva, lakini angalau wao wanaweza kupata matamasha na kulipwa hata wasipouza Dvd.
Suala linakuja kwetu watu wa filamu tukishindwa kuuza filamu katika Dvd tutafanya nini ili maisha yaendelee? Maana siku hizi hakuna tena maigizo ya jukwaani kama zamani na tunahitaji sana sanaa ya maigizo katika majukwaa ni muhimu.