Picha jinsi alivyochinjwaJeshi la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumuuwa dereva Bodaboda mmoja aitwaye Frenk Joseph (25)mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinja shigo na kisha kumpora pikipiki yake aina ya SANLG yenye namba za usajiri T 704 CDQ.
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote wakazi waTarafa ya Mwese Wilayani Mpanda.