Thursday, May 29, 2014

KUTANA NA JAMAA ALIYEMPA MWANAE JINA LA YESU INGAWA KANISA LIMEKATAA..SOMA HAPA!!

Ndiritu Njoka kwenye headlines tena wakati huu sio kukabiliana na Wanawake wanaowapiga Waume zao bali wakati huu jamaa anataka kanisa na Presibiteria ya Africa Mashariki-PCEA kumbatiza mwanae wa kiume aliempa jina la Jesus ama Yesu. Njoka amesema ameamua kumpa mwanae jina hilo kwasababu jina Yesu ni jina zuri sana >>’Sijamuita mwanangu kristo, nimemuita Yesu kwasababu ni jina nzuri sana’
 Njoka pia amedai kwamba kanisa na hata hospitali aliyozaliwa mwanae wamekataa kumuandikia cheti cha taarifa ya kuzaliwa kwasababu hawataki kuandika Jina Yesu kwenye cheti hicho.
 Njoka alipoulizwa kuhusu hilo amesema >>’hata kama hospitali walikataa kuandika hilo jina Yesu, nitatumia mkono wangu kuandika hiyo taarifa ya kuzaliwa Yesu Njoka kwasababu huyo ni mwanangu’.
 Rais huyo wa Wanaume ambae amekua akihusika na chama cha kutetea haki za Wanaume duniani ameongeza kuwa ameacha kwenda kanisani kwa sababu ya kukataa kumbatiza mwanae Yesu >’nimewaambia sawa basi hata hayo mambo ya kanisa nitaacha na nitakua nikiomba nyumbani kwasababu kama shida ni kumwita mwanangu yesu si lazima niende kanisani’

 Screen Shot 2014-05-28 at 2.25.36 PM
Nae katibu mkuu wa kanisa hilo la PCEA Kasisi Thegu Mutahi anasema jina la Yesu hawezi kupewa mtu maana Yesu ni mwana wa mungu >>> ’ukimuita mtoto yesu unamwona hapo barabarani akicheza na wenzake anaitwa Yesu !, Yesu !, Yesu ! hilo jina na tunajua yesu ni mwokozi litachukuliwa vipi?’.
 Aidha Njoka amesema amekerwa na hatua ya kanisa kukataa majina mazuri wakati wananyamazia watu wanaojiita Mwashetani na wengine Mwakaburi ambapo kwa sasa Njoka amesema amemuandikia barua Papa wa kanisa Katoliki kama njia ya kutafuta kibali kumuita mwanae Yesu Njoka Njoka.