Monday, May 26, 2014

MWANAMUZI KHALID CHOKORAA AINGIA RAMI KWENYE MCHEZO WA NGUMI..TAZAMA VIDEO YA PAMBANO LAKE

Screen Shot 2014-05-26 at 3.41.38 AM
May 23 2014 mwanamuziki kutoka kundi la muziki wa dance Tanzania Mapacha Watatu Khaleed Chokoraa ambae ni mshindi wa tuzo za KTMA pia, alitangaza rasmi kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kwamba pamoja na kufanya muziki, sasa ni ramsi kwamba kazi yake nyingine mpya itakua ni ngumi za kulipwa ulingoni.
Kwa karibu miaka 7 anasema amekua akifanya mazoezi kujiweka sawa kimwili na kujiandaa kuwa bondia manake alikua anaona ndoto hii lazima itimie.
Kweli imetimia May 24 2014 ambapo alipambana na bondia kutoka Tanga (96.0 CloudsFM) Abdul Manyenza ambae alipigwa na Chokora kwenye round ya kwanza tu na hivyo msanii huyu kuvunja rekodi aliyoitangaza AMPLIFAYANI kabla kwamba anataka kupiga mtu kwenye round za kwanzakwanza tu