Saturday, May 31, 2014

NI MARUFUKU KUVAA KATA 'K' SUMBAWANGA....UKISHIKWA NI BAKORA TU!!

kata k
MKUU wa Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Mathew Sedoyeka amepiga marufuku kwa kijana yeyote wa kiume mahali popote wilayani humo kuvaa suruali kwa staili ya Kata K.
Pia aliwaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa , Vijiji , Kata , Tarafa na Wilaya kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama katika maeneo yao ya kiutawala kuwachukulia hatua kali vijana wowote wa kiume watakaobainika kuvaa suruali zao kwa staili hiyo ya Kata K.
Alitoa maagizo hayo hivi karibuni akihutubia mikutano mbalimbali ya hadhara wilayani humo.
kata k3
Alisema tabia hiyo ya vijana wa kiume kuvaa suruali zao kinyume cha utaratibu haiwezi kuvumilika kwa kuwa inatukanisha jamii.
Sedoyeka alionya Watanzania hususani vijana kuachana na tabia ya kuiga kila kitu kutoka nje ya nchi ikiwemo uvaaji wa nguo zisizo na staha kwa kuwa hauendani kabisa na mila na desturi pia maadili ya Kitanzania.