Monday, May 26, 2014

RAY C ATANGAZA KUMUOKOA VIDEO QUEEN MAARUFU "WA NYIMBO YA NOORAH-ICE CREAM" ALIYETUMBUKIA KWENYE MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Unaikumbuka nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri iliyotamba miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka ambapo ndani yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la Doreen. 

Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa.

Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram dakika chache zilizopita kuwa ”rayc1982 Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya,nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!namshukuru Mungu Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia doren Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!ikawa Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doren Kwa Mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!!am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani.

God We Trust!!!I love You my lil sister…..Nawahamasisha wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu uweze kusaidiwa!usikubali Maisha ya utumwa wa madawa ya kulevya,njoo tukusaidie…Ray C Foundation pamoja na Kitengo cha Methadone We love you guys,We can help you….”