Sunday, June 8, 2014

Baada ya Diamond, Vanessa Mdee kawa Verified Twitter

vanesa
Imekuwa kama zali jana, ikiwa ndio siku ya kukumbuka siku yake ya kuzaliwa, mwanamuziki na mtangazaji maarufu, Vanessa Mdee aka VeeMoney kaingizwa kwenye orodha ya watu maarufu duniani, kwa account yake ya mtandao wa kijamii wa twitter kuwa Verified.
 
Ni wasanii wachache sana hapa afrika ya mashariki waliopata bahati hii ya kujulikana kimataifa na kuweza kuwa verified katika mtandao huo wa kijamii.
 
Kwa wale ambao hawajui maana halisi au umuhimu wa account ya mtu kuwa verified  kwenye huo mtandao wa kijamii wa twitter  ni  kuwa   watu wengi wamezoea kufungua account feki.

Tatizo hili linawakuta watu maarufu na mara nyingi huzushiwa mambo mengi bila kujua kama ni account yake ya kweli au la, hii inasaidia kwa watu maarufu wenye wafuasi wengi kupata uhakika kuwa hii ndio account yake  au  la..