Monday, June 30, 2014

MANENO MAZITO ALIYOYATOA DIAMOND BAADA YA MSHINDI WA TUZO ZA BET KUTANGAZWA KUWA NI DAVIDO

Screen Shot 2014-06-29 at 9.53.47 PMDakika kadhaa baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu wake.
‘Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo, katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport’

Screen Shot 2014-06-29 at 9.45.57 PM