Thursday, June 26, 2014

MWANAMKE AJISOKOMEZA UKENI GRAMU 685 ZA MADAWA YA KULEVYA WAKATI AKIJARIBU KUYASAFIRISHA!!

Wakati anazungumzia kilichomsababisha ajiingize kwenye kazi hiyo alisema ni ugumu tu wa maisha ndio sababu kubwa.
Alisema hakuweza tena kuwahudumia watoto wake wanne ambao walikuwa wametelekezwa na baba yao mzazi, kulipa kodi ya nyumba nayo ulikuwa mtihani.
Akizungumzia jinsi alivyokutana na jamaa aliyemshawishi kufanya biashara hiyo alisema kuwa, aliahidiwa kusaidiwa kutatua matatizo aliyonayo na kweli jamaa alifanya hivyo huku akimhahidi kumpa biashara ya kusafiri.
Baadae alipokuja kujua ni biashara ya kusafirisha madawa, dada huyo alikataa kuifanya lakini alipata vitisho vikali toka kwa jamaa aliyemgharamia na kumtaka arudishe gharama zake.
Hakuwa na jinsi, hakuwa hata na senti tano nyeusi ya kulipa, basi ikambidi afanye biashara ndipo ikambidi ashindie gramu 685 za unga ukeni.
Ni mwanamke wa kinaijeria Chinelo Okorom, 36, muuza chakula mitaani aliyekamatwa katika uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed International Airport huko Ethiopia alipokuwa akisafirisha unga toka Nigeria kuingiza Ethiopia, unga aliokuwa ameushindia ukeni. Brimtime