Monday, September 22, 2014

DUH! NORA AJUTA KUWAHI KUOLEWA...NI BAADA YA KUOLEWA NA MGANGA WA KIENYEJI

 Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ akipozi.

MAJUTO! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa siku zote katika maisha yake anajuta kuolewa mapema kwani asingefanya hivyo angeweza kufanya mambo mengi na angekuwa mbali sana kisanii na kielimu. 

 

Nora alisema kuwa kipindi alipoolewa na aliyekuwa mganga wa tiba za asili, marehemu Ngwizikulu Jilala, alikuwa akimnyima uhuru wa kuendelea na sanaa na masomo.
“Unajua kweli najuta sana mimi kuolewa mapema kama si hivyo ningeendeleza fani yangu na sasa ningekuwa mbali lakini kipindi chote cha ndoa nilisimama sikuweza tena kuigiza,” alisema Nora.
Msanii huyo amesema kwa sasa amerudi upya kwenye gemu na tayari ameandaa sinema mpya inayokwenda kwa jina la Msimamo Wangu ambayo imeshakamilika, itatoka hivi karibuni.