Tuesday, June 24, 2014

NUH MZIWADA: UTAFICHA WAPI SURA YAKO SHIOLE AKIKUPIGA CHINI?


Siku chache baada ya mpenzi wa Zuwena Mohamed 'Shiole'  Nuhu  Mziwanda  kuweka kwenye mtandao   wa  'instagram' picha zikionyesha tatoo aliyojichora yenye jina la mpenzi wake huyo, wadau wa filamu nchini wamesema kijana huyo atakuja kujuta siku akitemwa na kubaki na alama zake hizo kama kumbukumbu.

Wakizungumza na mwanahabari  wetu kwa nyakati
tofauti, wadau hao walisema kuwa Shiole aliwahi kusema  kuwa yeye huwa anaacha wanaume na hajawahi kuachwa hivyo kitendo cha Mziwanda kudatishwa na penzi la msanii huyo, siku akitemwa atatamani kuikata miguu yake aliyoichora neno 'shishibaby' aliyodai haiwezi kufutika maisha yake yote.

''Kijana kashikwa pabaya na shishi baby wake, ngoja tuone hii muvi nayo itaishia wapi maana shilole alishawahi kusema yeye ameshawazoea kuacha na si kuachwa hivyo penzi lao likiingia dosali atatemwa na kubaki na majuto ya kuwa na tattoo hizo'' alisema mdau  mmoja  huku  akigoma  kuanikwa  jina  lake.

Mdau  Mwingine alisema ni kweli kwa sasa anaweza kuona sifa  kuwa na alama hizo kwa sababu penzi lao bado liko moto lakini atambue mapenzi huwa yanachuja na kama watu wako nje ya ndoa kuachana huwa si jambo gumu na kila mmoja kuanza maisha yake mapya.