Sunday, June 22, 2014

SKENDO ZASABABISHA AGNESS MASOGANGE AKIMBIE NCHINI....SOMA ZAIDI!!

Siku chache baada ya Agness Gerard ‘Masogange’ kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwa kile alichodai ni kutafuta maisha mazuri, rafiki wake wa karibu  aliyejitambulisha kwa jina la Jenifer  ameibuka na kuweka kila kitu hadharani juu ya nini kilichomkimbiza mrembo huyo
Jennifer alisema kuwa kilichomuondoa nchini mrembo huyo  ni vidole vya watu ambao wamekuwa wakimnyooshea kila alipopita kuhusiana na skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Jennifer alisema kuwa kitendo  hicho kilikuwa kikimkera na kumkosesha raha Masogange hivyo akaona njia rahisi ya kuondokana na hilo ni kuhama jiji kwa muda mpaka watanzania watakapoisahau skendo hiyo ndipo atarudi.
MASOGANGE2
Si kweli kwamba Masogange ameamua kwenda kuishi Afrika ya Kusini kwa kupenda, bali vidole vya watu waliokuwa wanaoneshana kila sehemu alipokuwa anapita kwani wengi wanamfahamu na alivuma na skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya Afrika Kusini hali ambayo ilikuwa inamnyima raha na kuona njia sahihi ni kuhama kwa muda Tanzania.” alisisitiza Jennifer.


Muda mfupi kabla ya kuondoka nchini, Masogange alisema kuwa ameamua kuhamia huko ambako anahisi ndiko maisha yake yalipo na mipango mingi ya kimaisha anafanikiwa kuliko Bongo.