Friday, July 18, 2014

ARSENAL YATAMBULISHA KITASA KIPYA CHA KUZIBA PENGO LA SAGNA

KLABU ya Arsenal imemsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Ufaransa, Mathieu Debuchy kutoka Newcastle wakati Washika Bunduki wakiendelea kumwaga fedha kusajili.
Debuchy, mwenye umri wa miaka 28, amechukuliwa ili kuziba pengo la Mfaransa mwenzake, Bacary Sagna aliyehamia kwa mabingwa,  Manchester City mapema baada ya msimu.
Arsenal iemtweet picha ya Debuchy ikiambatana na ujumbe#KaribuDebuchy.
Tangazo: Arsenal imetoa tangazo la usajili mpya