Saturday, July 19, 2014

BOB JUNIOR NAYE AFIKIRIA KUTEMBELEA NYOTA YA DIAMOND PLATNUMZ

Msanii wa muziki na producer, Bob Junior amesema kuna uwezekano mkubwa 
wa kufanya kolabo na msanii aliyemtoa, Diamond Platnumz.
Akizungumza na Bongo5, Bob Junior aliyetayarisha nyimbo za Diamond zikiwemo ‘Kamwambie’ na ‘Mbagala’ amesema kwakuwa yeye ndiye aliyemtoa akiamua muda wowote wanaweza kufanya naye kazi. 

“Kwa sababu nia bado ipo na sisi tupo hai hatuwezi kujua nini kitatokea, siwezi sema natamani ni kijana wangu ambaye nimemtoa mimi nikiamua siku nafanya naye nitafanya naye, haiwezi kuwa na ugumu,” amesema Bob Junior