Friday, July 11, 2014

HIZI NDIZO HELA ATAKAZOPATA BINGWA WA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU 2014.

Bingwa mara tatu Ujerumani na bingwa mara mbili Argentina wa fainali za kombe la dunia, watawania dola za kimarekani milioni 35 kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia siku ya Jumapili, Julai 13 mjini Rio De Janeiro.

Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa jumla ya dola za kimarekani milioni 576 kushindaniwa kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu, ambazo zitafikia tamati nchini Brazil mwishoni mwa juma hili.
Bingwa wa fainali hizo atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani milioni 35, mshindi wa pili atapata dola za kimarekani million 25, mshindi wa tatu atazawadiwa dola za kimarekai million 22 na mshindi wa nne ataondoka na kiasi cha dola za kimarekani million 20.
Timu nne zilizoondolewa kwenye hatua ya robo fainali kila moja itapokea dola za kimarekani million 14, timu nane zilizong'olewa katika hatua ya 16 bora kila moja itapokea kiasi cha dola za kimarekani milion 9 na timu zilizotolewa kwenye hatua ya makundi kila moja itachota kiasi cha dola za kimarekani million 8.
Jumla ya timu 32 zimeshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka huu na michezo takriban 64 itakamilishwa siku ya jumapili huku wachezaji walioshiriki wakiwa na timu za mataifa yao huko nchini Brazil walikuwa ni 736.
Ikumbukwe kuwa timu ya taifa ya Ujerumani imefuzu kucheza mchezo wa hatua ya fainali baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Brazil mabao 7-1, ili hali timu ya taifa ya Argentina ilitinga katika mchezo huo baada ya kuing’oa timu ya taifa ya Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-2.
Miongoni mwa wachezaji nyota kwa upande wa Ujerumani ni mfungaji bora kwa wakati wote wa fainali za kombe la dunia Miroslav Klose huku Argentina wakijivunia Lionel Messi mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani mara nne