Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.Alisema sangoma huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia mwanagu.
Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.“Pia nilikwenda Kituo cha Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba huyo.
Mzazi huyo aliiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande wake, muuguzi wa zamu aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Kwa ujumla huyu mtoto amebadilishiwa staili ya maisha na hicho ni kilema. Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika maisha yake,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.