Saturday, July 19, 2014

MONALISA AAMUA KUMFANYIA SUPRISE MAREHEMU TYSON...NI IPI IYO SOMA MWENYEWE!

STAA wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amefunguka kuwa bado anamkumbuka sana aliyewahi kuwa mumewe, marehemu George Tyson hivyo atafanya kitu kwa ajili ya kumuenzi.
Staa wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Akizungumza na mwandishi wetu siku ya Arobaini ya Tyson, Monalisa alisema daima ataendelea kumkumbuka na kumuombea Tyson na ameona kuna umuhimu wa kufanya kitu ambacho kitakuwa kumbukumbu maalum ya marehemu ambacho ni siri yake.
“Kifo cha Tyson ni kama vile sinema, daima namuombea nakumkumbuka siku zote. Siku chache baada ya hii Arobaini, nitafanya kitu ili kumuenzi,” alisema Monalisa.
Arobaini ya Tyson aliyefariki kwa ajali ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa, Yombo-Buza jijini Dar.