Hatimaye mwimbaji wa miondoko ya R&B wa nchini Marekani, Mya, amejibu tuhuma nzito zilizokuwa zimeelekezwa juu yake kuwa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rapa Jay Z nyuma ya mgongo wa Beyonce ambaye ni mke halali wa Jay.
Siku za hivi karibuni taarifa zilisambaa mitandaoni zikimtaja Mya na Jay Z kuwa na mahusiano ya siri kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mya amekasirishwa sana na tuhuma hizo na kucharukia mtandao ulioandika na kuvumisha taarifa hizo akisema sijawahi,sipo na sitawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Jay Z wakati akimjibu mmoja wa mashabiki wake kupitia Instagram.