Inasemekana kuwa huyu mtoto ameuliwa na baba yake mzazi kwa kipigo kikali...maeneo ya Moshi Vijijini- kijiji cha Mero...
Yaani ukiangalia Hata picha zake zinaonyesha kabisa jinsi mwili wa huyu mtoto Malaika ulivyojaa makovu ambayo ni ya kipigo cha mara kwa mara.....Yesu turehemu...
Inasemekana mtoto anakaa na baba yake mzazi na mama wa kambo... Ebu angalia jinsi huyu mtoto alivyoumizwa jamani..... yaani nimelia kwa uchungu maana huyu mtoto ameteseka sana kufa kwake.....alitamani mtu aje amkamate baba yake ili asiendelee kumpiga lakini hakutokea....alilia sana ili baba amuache lakini bado akaendelea kupigwa sana.... aliona jinsi baba anavyomuonea kwa kuwa yeye sii mkubwa kama baba yake hata ajitetee kwa kumzuia (mfano watu wazima wanavyopambana)

Mwili wa mtoto umeviria damu kwa kipigo toka kwa baba yake mzazi ambae nimeambiwa anaitwa Morsi Clemence, na mara nyingi shughuli zake ni vibarua vya hapa na pale...... Natamani sana kufanya kampeni maalumu ya ''OKOA MTOTO'' ili jamii iwalinde watoto wetu...
Tukio hili limetokea eneo linaloitwa kitu kama kwa ''Raria'' ambapo ni katikati ya njia panda na kabla hujafika Moshi mjini.... jamani huyu baba naskia amekimbia baada ya kujikuta ameua mwanae kwa kipigo kizito... Marehemu kazikwa jana baada ya babu mtoto kusema azikwe wakati baba mtoto (mtuhumiwa) akitafutwa popote alipo....
Mbaya zaidi nimeambiwa kwamba huyu baba ana mke ambae ni mama wa kambo na huyu mtoto ambae ndiye aliyekamatwa baada ya mume wake kukimbia kusikojulikana....