Monday, August 18, 2014

AISHA MADINDA SASA APATA SHAVU LA KWENDA KUYAKATA MAUNO DUBAI..AACHANA NA TWANGA PEPETA

Mkata mayenu wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Aisha Madinda amekula shavu la kwenda kunengua Dubai na kuachana na bendi hiyo kwa muda.Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya bendi hiyo, Aisha alikuwa ameshaanza kufanya mazoezi lakini hivi karibuni amekwenda Dubai kwa ajili ya kucheza shoo.
Mkata mayenu wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Aisha Madinda akiwa kazini.
“Unajua wanenguaji wengi huwa wanachukuliwa na kwenda kucheza shoo Dubai na wanalipwa vizuri, sasa Aisha amepata bahati hiyo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo mwanahabari wetu alimtafuta mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Aisha alikuwa hajaanza kazi rasmi lakini alikuwa anakuja mazoezini kila mara hivyo kuhusu kwenda Dubai hakuniaga mimi ila nasikia yupo huko.”
Naye kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu alithibitisha kwamba ni kweli Aisha yupo Dubai alikokwenda kwa ajili ya kucheza shoo na aliwaaga kwamba amepata shavu hilo.