Tuesday, August 26, 2014

HATIMAYE NICKI MINAJI AVUNJA REKODI HUKO YOU TUBE

nicki-minaj-anaconda-drake4_zps4c0de61c
Video mpya yenye utata kwa kwa baadhi ya nchi fulani kuzuiliwa kupigwa “Anaconda”, imevunja record ambayo mara ya mwisho ilikuwa inashikiliwa na video za mwanamuziki Miley Cyrus za ku-twerk stejini, Video ya anaconda inashikilia record mpya kabisa kwa kuangaliwa na watu milioni 19.4 duniani nzima ndani ya masaa 24 tu toka ilipoachiwa hewani kwenye mtandao wa Youtube.
Hii ndio inasemekana moja ya video zenye picha za wakubwa zaidi mwezi huu,wengi wanadhani kuwa kutokana na kupewa promo nyingi katika mitandao mbali mbali kabla haijatoka ndio imesababisha kuvunjwa kwa record hii, ila wadau wa muziki wanasema kuwa video hii ni nzuri na imegusa haswa maudhui ya mwandishi na ndio maana imepokelewa vizuri na wapenzi wa muziki.