<<Mara ya kwanza ilikuwa kwenye social network tu.. nilikuwa namuonaona tu napita kwenye page yake na-like.. nilitoka kushoot video ya ‘Coco Baby’ South Africa tukakutana kwenye ndege..>>—Diamond Platnumz anasimulia walivyokutana na mpenzi wake Zari kwa mara ya kwanza.
Kumbe hiki ndicho kilimvutia sana Zari kwa Diamond Platnumz>> “Ni mchangamfu.. anajali.. Diamond ana akili sana, nilivutiwa nae kwa sababu ana akili sana.. anajituma sana, ni mtu mwenye malengo makubwa..”>> —Zari.
Kwani Diamond amewahi kuonana na watoto wa Zari?? Wanamchukuliaje? >> “Bado hawajawahi kuonana.. ila watoto wanamjua.. kama mama yao nina furaha wao wana furaha pia>>—Zari.