NYOTA wa filamu Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amesema anajihisi kama mwanamke
mwenye mkosi baada ya wanaume wanne alioshiriki nao mapenzi kuonesha nia
ya kumuoa, lakini ghafla waliingia mitini na kupeperusha ndoto yake ya
kuwa mke wa mtu.
Akipiga stori na gazeti hili, muigizaji huyo alisema umri wake
unamruhusu kuolewa na anafanya kila njia ikiwa ni pamoja na kutii
maelekezo yote ya mwanaume ili kumvutia aingie naye katika ndoa, lakini
kinachomshangaza hubadilika ghafla na kumpotezea kabisa.
“Siyo siri naumia sana, huenda nimerogwa nisiolewe, mwanaume
anajitambulisha hadi kwa wazazi na kuanza mchakato wa ndoa lakini
baadaye anaingia mitini,” alisema Rayuu