Thursday, August 28, 2014

KALAMA ‘AMNYOA’ NYWELE BELA

MWANADADA anayeunda Kundi la Scorpion Girls,Isabela Mpanda ‘Bela’ amejikuta akinyoa nywele baada ya mpenzi wake wa siku nyingi, Luteni Karama kumtaka afanye hivyo.
Mwonekano mpya wa mwanadada anayeunda Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’.
Bela kwa sasa anaonekana katika mwonekano wa tofauti kabisa kwani amenyoa na kubaki na nywele fupi tofauti na alivyozoeleka ambapo alisema kwamba mpenzi wake ambaye wanatarajia kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu, Karama ndiye aliyemwamuru anyoe kwani hapendi nywele ndefu.
Isabela Mpanda ‘Bela’ akiwa na mpenzi wake 'Luteni Kalama' kabla ya kukata nywele.
“Imebidi ninyoe ili kumfurahisha mpenzi wangu Karama maana ninampenda kuliko kitu chochote hivyo lazima nimsikilize kwani yeye ndiye aliyenitaka nikanyoe,” alisema Bela.