Friday, September 26, 2014

AFANDE SELE AKANUSHA VIKALI KUTOKA NA MPENZI MPYA SIKU 1 BAADA YA 40 YA MAMA WATOTO WAKE



Rapper wa Morogoro, Afande Sele ameeleza kusikitishwa kwake na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku kuwa ameonekana na mpenzi mpya siku moja baada ya kupita arobaini ya mzazi mwenzake, Mama Tunda.
1184877_641324759317470_8644934034470494383_n
Afande ametumia Facebook kueleza ukweli wa mambo.
Wakati flani katika maisha sisi wanasanaa na waandishi wa habari tunahitilifiana kwa kutokuheshimiana tu; na kwa hakika kama tungetanguliza heshima miongoni mwetu daima tusingekwaruzana hata kidogo ukizingatia kuwa tasnia zetu zinategemeana sana,hebu angalia muandishi kama huyu anatumia picha yangu mimi na dada asiemjua halafu bila kuniuliza mimi kama muhusika kuwa huyo dada ninani na anauhusiano gani namimi yeye muandishi moja kwa moja anapeleka picha kwenye mitandao/magazeti na bila aibu,woga na kuheshimu tasnia yake anaandika kuwa’siku moja baada ya 40 ya mkewe afande anamwanamke mpya’ wakati si kweli,” ameandika Afande.
“NIMEFAIDHAIKA SANA!, ukiachilia mbali suala la kunidhalilisha katika jamii au kunitia ubaya mbele za watu kwa kunisingizia kuwa nimekutwa na mwanamke siku moja baada ya arobaini ya mzazi mwenzangu bado pia sijui hasa huyu muandishi dhamira yake kuu ya kutumia picha hiyo ya kawaida na kuitungia habari ya uongo kama hiyo ilikuwa nini?au ndio tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu?chondechonde ndugu wanahabari kalam zenu mkizitumia vibaya huwa ni silaha nzito kuliko ndege za kivita za jesh la marekani,kwa imani ya dini yangu hata kabla ya kifo cha mzazi mwenzangu ningeweza kuruhusiwa kufunga ndoa na bint mwingine hasa ukizingatia mimi na mama wa hasa ukizingatia kuwa mimi na mama watoto wangu tulikuwa tumeshatengana mwaka mmoja kabla hajafikwa na umauti, lakini kwangu mimi bado sikuwa na sina wazo hilo la kuoa.”