Wednesday, September 10, 2014

BI MWENDA AMEMTAKA RAIS AJIUZULU

MKONGWE wa uigizaji Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ amemtaka Mwenyekiti  wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ asijiuzulu kwani kazi aliyoifanya hadi sasa ni kubwa na nzuri.
Mkongwe wa uigizaji Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’
“Mimi nashangaa haya maneno yanatokea wapi sijui, lakini sipendi kusikia Steve Nyerere amejiuzulu na kama akijiuzulu, atakayekuja hawezi kuwa kama yeye ni mtu wa watu, hachagui habagui,” alisema.Mwenyekiti  wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Aidha alisema katika kipindi cha uongozi wake, klabu yao imekuwa na maendeleo makubwa.
“Katika viongozi waliopita hakuna hata aliyeleta maendeleo ya klabu yetu zaidi ya majungu tu, hata hivyo mimi naona Steve yuko sahihi sielewi wenyewe wanajifikiriaje,” alisema.