Kitendo cha kutojaaliwa makalio makubwa kwa staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti kimemsababishia anangwe na wasanii wenzake.
Akiongea na mwandishi wetu, Esha alisema anafahamu na anawashangaa watu wanaoponda maeneo hayo ya mwili wake kwani kwa upande wake anaamini kuwa mwanamke sura, makalio majaaliwa kwani hata mwanaume aliyemuoa analijua hilo na anampenda jinsi alivyo.
“Kwa kuwa mume wangu ananikubali jinsi nilivyo hainiumizi kichwa kwani mimi naamini sifa ya mwanamke ni tabia na wala siyo shepu kama wengine wanavyofikiria,” alisema Esha.