Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi.
Mpango mzima ulijiri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, wikiendi iliyopita ambapo katika kuonesha ubunifu, mchekeshaji Joti, alitupia vazi la jinsi zote ambalo upande mmoja lilionekana ni sketi ya kike na mwingine suruali ya kiume.Kama hiyo haitoshi, mwili wake aliugawa katika nafsi hizo mbili kwani licha ya sketi, pia mguu wake wa kushoto alivaa kiatu cha kike, kama ambavyo kichwani kwake, alisuka nywele upande mmoja kama mdada.Kitendo hicho kilionekana kama kuwapa bichwa wanaume wenye kufanya mapenzi ya jinsia moja, kwani waliona ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kuvaa mavazi ya kike.
Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akitumbuiza jukwaani ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alivaa kivazi kilichoonesha sehemu kubwa ya mwili wake, kikiwa kimeziba matiti kwa mbali na kusababisha wanaume wakware kutokwa na udenda.Katika fainali hizo za kumsaka mwenye kipaji cha kuigiza ukumbini hapo, mshiriki kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu ndiye aliyeibuka mshindi na kuondoka na cheki ya Sh. milioni 50.
LULU AINGIA UKUMBINI
Shushushu wetu alimshuhudia Lulu akizama ukumbini humo akiwa amevalia gauni hilo lililoacha wazi sehemu ya mwili wake hivyo kujichafua mbele ya mamia ya mashabiki waliohudhuria.
“Yaani Lulu huwa anaonekana kama hajali vile, hebu muone nguo aliyovaa, imemuacha wazi sana, karibu mwili mzima uko wazi na anatangaza kwa kujiamini mpaka dah! Ni balaa!” alisikika mmoja wa wahudhuriaji hao.
‘Joti’ akizidi kuwaonyesha vimbwanga vya 'kikomedi' watazamaji waliohudhuria fainali za TMT ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alionekana kujiamini kupita kiasi bila kujali macho ya watu kwani alifanya kazi yake vizuri na hakuwa na wasiwasi wowote kufuatia nguo aliyokuwa ameivaa mwanzo.JOTI NAYE
Kufuatia kipaji alichonacho, Joti, kila mtu hakuamini pale alipopanda stejini kutumbuiza kwa staili ya aina yake kufuatia vazi lake alilokuwa amevalia yaani nusu mwanaume na kuwafanya watu washindwe kukaa na kuishia kuangalia shoo aliyokuwa akiitoa kwa mashabiki.
“Ama kweli watu wana vipaji vyao, yaani kwa wakati mmoja Joti ameweza kuigiza kama mwanamke na mwanaume. Ukiachana na hayo, hadi nguo nayo imeshonwa hivyo! Dah! Fundi alifanya kazi tena nampongeza sana Joti maana nilijua anakuja kuigiza,” alisikika mhudhuriaji mwingine.
Katika maelezo yake, Joti alisema sababu ya kufanya vile ni sapraizi tu kwa mashabiki wake kwani huenda walijua atakuja kama ambavyo huwa anafanya sehemu mbalimbali.
“Nimeamua kuja kivingine, hii staili ni ya kawaida tu, sema watu wameshangaa kuniona vile, ndiyo maana Lulu alisema ni sapraizi kwa mashabiki, ni kweli nimewafurahisha sana na huwa wanashindwa kunielewa kwa jinsi ninavyobadilikabadilika,” alisema Joti.
Joti hakuishia hapo kwani baada ya mshindi kutangazwa tu, alitoa shoo ya nguvu huku watu wakimzunguka na kumuimbia kwa kufurahishwa jinsi alivyokuwa akicheza.
Kabla ya shindano hilo, Lulu na Joti waliwahi kudaiwa wanatoka lakini kwa pamoja walikanusha vikali skendo hiyo na kuweka hadharani kuwa uhusiano wao ni wa kikazi tu.