Monday, September 22, 2014

"SIWEZI KUWA NA WEMA SEPETU, KWA TABIA ZAKE NAWEZA NIKAMPIGA NGUMI MPAKA NIKAUA"....TUNDA MAN

MKALI wa kibao cha Msambinungwa, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’, amesema hana mpango wa kutoka kimapenzi na msanii wa filamu za maigizo, mwanadada Wema Sepetu kwa kuwa hawaendani kabisa.
Tunda Mana katika pozi na presenta wa Global TV Online, Pamela Daffa 'Pam D' wakati wa mahojiano hayo.
Akuzungumza na Global TV kupitia kipindi cha Mtu Kati, Tunda alisema kuwa hafikirii hata mara moja kama atakuja kutoka kimapenzi na staa huyo kwa kuwa watakuwa wanapishana kwenye baadhi ya mambo.
Tunda Man ndani ya studio za Global TV Online.
“Wema ni rafiki yangu kama walivyo marafiki wengine lakini kitu kikubwa sitamani kabisa aje kuwa mpenzi wangu kwa sababu tutakuwa tunapishana katika baadhi ya mambo na hizi ngumi ninazocheza nahisi nitampiga mpaka nitauwa,” alisema Tunda Man.