Thursday, September 25, 2014

MKWE WA OSAMA BIN LADEN AHUKUMIWA KIFUNGO CHA JELA MAISHA NA MAHAKAMA YA NEW YORK.

 
Mkwe wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda , Osama bin-Laden amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama moja mjini New York. Alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi.

Jaji wa mahakama hiyo amemwambia Suleiman Abu Ghaith kuwa alionekana kuwa na nia na tayari kutekeleza ajenda ya mauaji kwa niaba ya al-Qaeda'

Suleiman Abu Ghaith mwenye umri wa miaka 48, alifanywa kuwa msemaji wa Al Qaeeda baada ya shambulizi la 9/11 na anasemekana kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Al Qaeeda kufikishwa mahakamani Marekani tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.

Alikamatwa nchini Jordan mwaka jana na kupelekwa Marekani alikokabiliwa na mashitaka hayo.  

Pia alitetea kazi yake akisema ni jukumu lake la kudini kuwaambia waisilamu wapambane na maadui wao 

Mnamo mwezi Machi, jopo la majaji wa kiraia lilimpata na hatia ya njama ya kuwaua wamarekani pamoja na kulisaidia kundi la al-Qaeda.

Kanda za video zinazomuonyesha Abu Ghaith akitoa vitisho dhidi ya Marekani akisema analenga kuangamiza Marekani kwa kutumia ndege zilionyeshwa kwa majaji hao.

Abu Ghaith alisema kuwa jukumu lake ni la kidini kwani alikuwa akiwaaasa waisilamu kupambana na maadui wanaowakandamiza.