Monday, September 29, 2014

PICHA PICHA ZNATISHA.. MTUHUMIWA APIGWA MOTO BAADA YA KUSHINDWA KUJIELEZA

baada ya kushindwa kujieleza juu ya pikipiki
ambayo yeye na mwenzake walikuwa
wanajaribu kuiuza Chalinze.
Watu hao walifika Chalinze wakidai kutokea
Gairo wakitaka kuuza pikipiki aina ya Toyo
yenye namba za usajili T 336 BZC.
Lakini walipobanwa kuhusu kadi ya pikipiki
walibabaika na hivyo kuanza kupigwa ambapo
mmoja alitoroka na huyo mwingine kuuawa kwa
kuchomwa moto baada ya kipigo.
Tukio hilo limethibitishwa na kaimu kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athuman
Mwambalaswa.
Kamanda huyo alisema kwamba tukio hilo
lilitokea Septemba 25 mwaka huu, majira ya
saa 1 asubuhi eneo la Pera Chalinze wilaya ya
Bagamoyo.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha
kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume
cha sheria na kuwataka kuwapeleka kwenye
vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na polisi ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.