Friday, October 9, 2015

KIWANDA CHA KUSINDIKA SEHEMU NYETI ZA NG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM


Hatimaye, Halmashauri ya manispaa ya Ilala imekifunga rasmi kiwanda bubu kinachosindika sehemu nyeti za Ng'ombe Dume, kutokana na kufanya kazi zao katika makazi ya watu,huku kukiwa na mazingira machafu na kusababisha harufu kali katika eneo la Tabata bima mtaa wa umoja jijini Dar es salaam.
Kufungwa kwa kiwanda hicho Bubu ambacho pia kimekuwa kikikusanya pembe za ng'ombe na kusafirisha nchini China, kumetokana na malalamiko kutoka wananchi ambao walikuwa wakilalamikia harufu kali, inzi na mazingira machafu ya eneo hilo.
Aidha wamiliki hao raia wa kichina pamoja na kufungiwa rasmi wamepigwa faini ya shilingi millioni kumi, kutokana na kuendesha shughuli zao katika mazingira machafu hali inayoweza kueneza magonjwa.
Mmoja wa wafanyakazi katika eneo hilo amesema nyeti hizo za ng'ombe zimekuwa zikiletwa na kukaushwa eneo hilo na baadae kusafirishwa kwenda china kwa ajili ya kutengeneza dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu Viagra.
Katika eneo hilo pia kimebainika kiwanda cha kutengeneza vitu mbali mbali vya ndani ikiwemo sahani za plastic huku zikiwa zimebandikwa lebo kutoka china ambapo baada ya kutakiwa kuonyesha vibali walishindwa kuonyesha na kudai kiwanda hicho kipo katika hatua za majaribio.