Pichani juu na chini ni umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia) na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga .
Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ukipenda muite Mr Blue,msanii wa muziki wa kizazi kipya juu ya jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.