Wednesday, September 3, 2014

VIDEO INATISHA: KUNDI LA ISIS LAMKATA KICHWA MWANDISHI MWINGINE WA MAREKANI, LATISHIA KUMKATA MWINGINE RAIA WA UINGEREZA KULIPA KISASI ( VIDEO INATISHA)


Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Iraq na Syria (ISIS) limetekeleza mauji mengine ya kutisha kwa kumkata kichwa mwandishi  mwingine wa habari wa Marekani.  

 
Mwandishi huyo aliyetajwa kwa jina la Steven Sotloff mwenye  umri  wa  miaka 31 alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
 
Katika video hiyo  iliyopachikwa  hapo chini, mwandishi   huyu  anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.

Sotloff  ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa:

'Obama, your foreign policy of intervention in Iraq was supposed to be for preservation of American lives and interests, so why is it that I am paying the price of your interference with my life?.''
 
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kiingereza anamlaumu Rais  Obama  kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
 
“I’m back, Obama, and I’m back because of your arrogant foreign policy towards the Islamic State..

 “As your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike necks of your people,anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
 
Muuaji  huyu  anasadikika  kuwa ni  yule yule  aliyemchinja  mwandishi  wa  kwanza mwezi  uliopita.
 
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake,muuaji huyo anaanza kumchinja Sotloff lakini video hiyo inazimwa .
 
Sekunde chache baadaye mateka mwingine raia wa Uingereza  David Cawthorne Haines, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa taifa la Marekani.
  
Tazama  Video  hapo  chini( Video  inatisha) .Video  hii  imeanza  na  hotuba  fupi  ya  Rais  Obama . Baada  ya hotuba  hiyo, Mwandishi  huyo  anawekwa  mbele  ya  kamera  na  kuuawa  kikatili.