Wednesday, September 3, 2014

VIDEO YA NEY WA MITEGO "MR. NAY" YAZUA GUMZO, MAMA YAKE MZAZI AMUITA AMUELEZEE VIZURI INA MAANA GANI..NI FREEMASON AU?

Screen Shot 2014-09-03 at 3.55.01 AMNay wa Mitego msanii wa bongofleva ambae yupo kwenye list ya watakaotumbuiza katika stage ya Serengeti Fiesta 2014 Ijumaa hii hapa 98.6 Musoma na Jumapili 87.5 Shinyanga, amethibitisha kwamba Mama yake mzazi amemuita na kutaka kujua kilichoonekana kwenye video yake mpya ya‘Mr. Nay’ aliyoifanya Kenya kinamaanisha nini.
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.10 AM
Nay ambae kabla ya kufanikiwa kimuziki aliwahi kuwa kinyozi wakati bado akisoma sekondari, ameongea na millardayo.com na kusema mama yake mzazi amemuita nyumbani September 2 2014 kutaka kujua kinachoendelea sababu alichoona na anachoambiwa na watu kimemfanya apate wasiwasi mkubwa.
Nay anasema ‘mimi nafanya kitu kutokana na idea ambazo huwa zinatoka kichwani mwangu, nafikiri watu wameona ni video kubwa nzuri na kali…. sijawahi kufanya video kali kama hii ambayo kidogo inataka kuniletea shida ila sio kitu kibaya kwangu’
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.24 AM‘Zile damu, na vitu vingine kama vya kishetani pamoja na namba ninayopenda kuitumia ya #966 ni vitu vinavyofanya nipate sana msg na kuulizwa maswali, na ndivyo vitu vimemshtua mama mpaka akaniita, watu wengine wanadhani mimi ni mwabudu shetani ila nataka watu watambue kwamba hakuna kitu kama hicho, ni ubunifu tu… na hii namba kuna siku nitakuja kuielezea maana yake hapahapa kwa millardayo
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.32 AMNay amesema ataweka wazi kila kitu alichoambiwa na mama yake baada ya kukutana nae kuzungumza kuhusu hii video ambayo imemuhuzunisha kama mzazi ikiwa ni video ya kwanza kumfanya amuite na kuhoji.