Mario Balotelli alionekana akivua bukta yake katika uwanja wa mazoezi wa Melwood
UTUKUTU wa Mario Balotelli usikie tu. Huyu jamaa ni noma sana.
Wakati mazoezi leo, nyota huyo mwenye miaka 24 alionekana kuhangaika na kaptula yake akiivua baada ya mazoezi na kubaki 'kichupi' nje.
Mshambuliaji huyo alibaki katika uwanja wa mazoezi wa Melwood wakati wa mapumziko kupisha mechi za kimataifa kutokana na kutumikia kifungo cha mechi moja.
Kifungo hicho kilimfanya asiitwe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Italia.
Mario Balotelli aliikosa mechi ambayo Italia walishinda mabao 2-0 dhidi ya Norway akitumikia kifungo cha mechi moja.
Hii sio mara ya kwanza Mario Balotelli kuwa na matatizo ya nguo
Mambo ya Balotelli hayo .