Thursday, September 11, 2014

MWANAMKE ABAKWA KISHA KUNYONGWA HADI KUFA NA KUTUPWA KICHAKANI HUKO MKURANGA

MKAZI wa Kijiji cha Bupu kata ya Bupu Tarafa ya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Forodesi Ntabegera (30) ameuwawa kwa kubakwa kisha kunyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Kwa mujibu wa taarifa ziliotolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP) Athuman Mwambalaswa Marehemu kuwa marehemu alinyongwa na watu hao kwa kutumia kitenge chake alichokuwa amekivaa.
Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana baada ya wakazi wa kijiji hicho kufanya msako wa kumtafuta marehemu ambaye alipotea Septemba 8.

“Baada ya msako huo kufanyika mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kichaka umbali wa mita 30 kutoka barabarani ambapo mwili wake ulimwagiwa unga sehemu za kichwani na mgongoni,” alisema Kamanda Mwambalaswa.

Alisema watu hao walitumia mfuko wa salfeti aliokuwa amebebea unga aliotoka kuusaga mashine, kumvisha miguuni kisha mwili wake waliulaza kifudifudi.

Aidha alisema kuwa taarifa za kupotea marehemu zilitolewa na kituo cha polisi Kimazinchana na mwenyekiti wa Kijiji cha Bupu Kasimu Kambangwa walioongozana na watoto wa marehemu ambao walidai mama yao alitoweka baada ya kuaga kuwa anakwenda kusaga na hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa kwenye eneo hilo.