
Soraja VucelicGazeti la udaku la Belgrade, Kurir limedai kuwa wawili hao walikutana mwaka jana huko Ibiza na wamekuwa wakiwasiliana kwa Skype. Gazeti hilo limedai kuwa Vucelic alikubali kumtembelea Neymar Barcelona mwishoni mwa October. Neymar aliamua kusitisha tiketi za ndege alizokuwa amekata Vucelic na kuamua kumtumia ndege binafsi ikamchukue yeye na rafiki yake. Mrembo huyo wa Serbia alidaiwa kukaa Barcelona kwa siku kadhaa.