Thursday, October 9, 2014

ASKARI WA USALAMA BARABARANI WALIOPIGA PICHA YA MAHABA WAKIWA NA SARE ZA POLISI WAFUKUZWA KAZI

Polisi Mkoani Kagera imewafukuza kazi Askari wake watatu kwa kuweka picha za mahaba kwenye mitandao ya kijamii. Askari hao walikuwa wanafanya kazi kikosi cha usalama barabarani Wilayani Missenye.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Henry Mwaibambe amesema picha hiyo sio ya kuchakachua na ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kwa kuwa kitendo hicho kimelidhalilisha jeshi la Polisi.
-jf