Thursday, October 2, 2014

BETHIDEI YA WASTARA TAMU, CHUNGU AMWAGA MACHOZI KATIKATI YA SHEREHE BAADA YA KUMKUMBUKA SAJUKI

BETHIDEI ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma imegeuka kuwa maumivu baada ya kumkumbuka aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ukumbini.
Shabiki akimpongeza Wastara kwa kumbeba mgongoni.
Sherehe hiyo ya kuzaliwa ya nyota huyo ilifanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wenzake wa filamu.
Wastara ambaye alionekana kama bibi harusi jinsi alivyopendeza, baada ya burudani ya muziki kupita, watu wote walisimama na kuomba dua kwa ajili ya marehemu wote akiwemo Sajuki, ndipo Wastara alipoingiwa na huzuni kubwa huku machozi yakimlengalenga baada ya kusikia jina hilo la marehemu mumewe.Wastara akisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na msanii mwenzake Stanley Msungu.
Kutokana na machozi hayo ya Wastara, ukumbi mzima ulizizima kwa majonzi kwa muda, baadaye burudani zikatawala kisha Wastara akapewa nafasi ya kuzungumza ambapo alimmwagia sifa za kutosha meneja wake, Bond Bin Sinan na kusema baada ya Sajuki kufariki, Bond ndiye amekuwa msaada mkubwa kwake.
Akipongezwa na meneja wake Bond Bin Sinan.
“Ukweli namshukuru sana Bond kwani kama siyo yeye nisingefika hapa nilipo, amekuwa akinishauri na kunisimamia katika kazi zangu za sanaa,” alisema Wastara.
Baada ya hapo, Bond naye alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo naye akammwagia sifa Wastara.
“Wastara ni mwanamke mwenye sifa za kuitwa mwanamke na ninajivunia kufanya naye kazi kwani anajitambua na anaelewa anachoelekezwa,” alisema Bond
Baadhi ya mastaa waliokwepo kwenye sherehe hizo.
Katika sherehe hiyo, msanii Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wake Chuchu Hans walikuwa kama kumbikumbi kwani waliingia wakiwa wameshikana mikono huku wakiitana mume, mke na kuzunguka pamoja wakiwa wameshikana viuno.
Mastaa kibao walihudhuria akiwemo, JB, Flora Mvungi, Sajent, Nisha, Mzee Chilo, Dude, Tito, Kupa, Cathy na wengine wengi huku upande wa burudani, mwimbaji wa Taarab, Amigo akitumbuiza.