Thursday, October 22, 2015

AIBU:MCHEZAJI WA SIMBA ANASWA NA HIRIZI KUBWA UWANJAN JANA HUKO MBEYA

Wachezaji wa Prisons wakimzonga mshambuliaji Msenegali wa Simba SC, Pape Abdoulaye N'daw kumshinikiza avue hirizi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Prisons ilishinda 1-0 
Mwishowe refa alimuamuru N'daw arudi kwenye chumba cha kuvalia akakaguliwe
N'daw 'akimtisha' mchezaji wa Prisons aliyemshupalia amevaa hirizi 
N'daw akiingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo ili kukaguliwa wakati ambao mchezo ulisimama kwa dakika nne kipindi cha kwanza
Watu 'waso haya' wanapiga chabo madirishani wakati N'daw anakaguliwa chumbani
 N'daw anarejea uwanjani baada ya kukaguliwa
Mchezaji wa Prisons aliyedai N'daw ana hirizi akionywa kwa kadi ya njano kabla ya mchezo kuendelea