Saturday, October 31, 2015

Rais Mteule, Dr. Magufuli Aikosoa CCM.....Awataka Wanafiki Walioko Ndani Ya CCM Wajisalimishe Mapema

Rais Mteule Dk John Magufuli ameamua
kufunguka kuhusu ugumu aliokabiliana nao
wakati wa mchakato wa kampeni akieleza kuwa
uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na
changamoto kubwa kutokana na hujuma
zilizofanywa na wanafiki waliojificha ndani ya
Chama cha Mapinduzi(CCM).
Amesema amekerwa na hali hiyo kiasi cha
kushindwa kuvumilia kuizungumzia jana, hasa
baada ya kuona uchaguzi umekwisha, hivyo ni
vyema wanafiki hao wakajisalimisha kwa
kutubu kwa kuwa wamekigharimu chama
hicho na kusababisha kiwe kwenye wakati
mgumu.
Amesema kwamba asiposema atakuwa ni
mnafiki kwa sababu uchaguzi umekwisha bora
wawekwe wazi kwa sababu anaona ni bora
kuishi na mchawi kuliko mnafiki, alimuomba
Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya
asiwahurumie wanaokihujumu, hivyo
kusababisha washindwe kufika kwenye
malengo.
“Nisiposema nitakuwa mnafiki msema kweli ni
mpenzi wa Mungu watubu wajirekebishe ni
mara kumi kuwa na mpinzani kutoka nje kuliko
ndani ya chama,mipango yenu mtaipanga
mchana usiku wataitoa nje ni afadhali uwe na
mchawi atakuroga ufe kuliko mnafiki ndani, ”
amesema Maguli katika hafla ndongo ya
kumpongeza baada ya kukabidhiwa cheti
na kuongeza:
“ Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli wewe ni
mwenyekiti lakini ulikaa na wanafiki ndani ya
CCM, ndiyo wametufanya wakati mwingine
tufike hapa tulipofika, ndiyo wametufanya
tufike hapa tulipo , leo kwa hiyo nakuomba
ukitengeneze chama chetu vizuri
ukishamgundua mnafiki usikae naye fukuza
kesho, nimeona hili nilizungumze lakini
unisamehe sana kwa sababu ningebaki nalo
moyoni ningenisababishia kiungulia,ambacho
nimekiona wakati nazunguka nikiwa kwenye
kampeni,”
Kuanza kazi haraka
Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa
mara baada ya kuapishwa siku hiyo hiyo
atanza kufanya kazi, kwa kuwa hakuomba
nafasi hiyo kwa majaribio bali kuwatumikia
wananchi kwa dhati.
Pia ameomba ushirikiano mzuri kutoka kwa
wananchi ili waweze kufanikisha yale ambayo
wameahidi wakati wa kampeni yeye na na
Makamu Rais Samia Suluhu Hassan, ili waweze
kutimiza wajibu wa kuwatumikia bila kinyongo
na kuyatimiza yake waliyoahidi wakati wa
kampeni.
“Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu watanzania
wote bila kujali vyama vyetu tunaomba sana
ushirikiano wenu , tusipopata ushirikiano wetu
hatuwezi kuyatimiza kwa wakati, tisipopata
ushirikiano mzuri kutoka kwenye
mtatuchelewesha mara unataka kufanya hizi
mara kuna maandamano yakashindwe,
yakalegee yakabaki huko huko yalikoanzia,
kwa sababu sisi tunataka tufanye kazi,” alisema
Dk Magufuli na kushangiliwa.
Aliongeza kusema“ Katika kuzunguka kwetu
kwa wananchi wameona kuna kero nyingi za
maji, umeme, miundombinu, wananchi
wanataka zitatuliwe haraka, niwaombe
watanzania bila kujali vyama naomba
ushirikiano wenu mzurI, ili tufanikishe hayo
tuliyoahidi wakati wa kampeni,” alisisitiza.
Amsifu JK
Rais huyo Mteule alimsifu Rais wa awamu ya
nne Dk Jakaya Kikwete akisema kwamba ni wa
tofauti kwani licha ya kumtembeza katika
maeneo karibu yote ya Ikulu , lakini pia
amekuwa na busara za kukubali na kuendeleza
madaraka ya kupokezana.
“ Nataka niseme mheshimiwa Rais una moyo
wa pekee, Mungu akujalie sana viongozi wengi
Afrika wanapokaribia kuondoka madarakani
wengine huwa wanatengeneza hata katiba
tofauti ili katiba ili waendelee kubaki
madarakani, lakini wewe upo tayari kuondoka
hata leo,” alisema.
Dk Magufuli alisema anaamini kwamba
wananchi wataendelea kumuombea, kumlinda
kwa kuwa amethamini Tanzania Kwanza, hivyo
ataendelea kuhitaji busara zake pale
itakapobidi atakapoingia madarakani.
Awali akitoa maoni yake mara baada ya Dk
Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi,
Mratibu wa Taifa wa ULINGO, Dk Ave Maria
Semakafu alisema anaamini wanawake wengi
wamefurahishwa na ushindi huo kwa sababu
kwa umewezesha pia kwa mara ya kwanza
katika historia ya nchi kuwa na Makamu wa
Rais mwanamke Samia Suluhu Hassan.
“ Tumefungua ukurasa mpya kwani miaka 20 ya
tamko la Mkutano wa wanawake Duniani wa
mwaka 1995 Beijing, tumekuwa na mrejesho
mzuri kuhusu mwitikio wa Serikali kuweka
ushiriki sawa wa nafasi za uongozi badala ya
kuwafanya wanawake wawe watu wa kupiga
kura kwa kuchagua viongozi wa ngazi
mbalimbali lakini sasa nao wanachaguliwa,
wanaaminika na kupewa nafasi kubwa ya
uongozi kama hii,” alisema Dk Semakafu .
Alisema uchaguzi wa mwaka huu umekuwa ni
wa kihistoria katika mambo mengi licha ya
ushindani wa kisiasa lakini wanawake wawili
walikuwa ni wagombea akiwamo Anna Mgwira
aliyekuwa akigombea nafasi ya urais kupitia
chama cha ACT Wazalendo.
“ Binafsi nilikuwa nafuatilia kwa karibu kampeni
zao kulikuwa na mwitikio mkubwa wa watu
walikuwa wakiwasikiliza na hakukuwa na hali ya
udhalilishaji wa kuona kwamba hawastahili kwa
sababu tu wao ni wanawake ,” alisema