Saturday, October 31, 2015

Zari Amvua Tiffah Hiziri iliyowekwa Mkononi Mwake na Bibi yake Mama Diamond

DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama
Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua
mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa
mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi
wabaki na vingi viulizo.
Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache
baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia
kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa
mila za Kibongo siyo tatizo.
Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi
huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’
hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, Zari
alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na
ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili
kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye
aliyefanya zoezi hilo.
Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa
miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida),
Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi
magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na
mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.
Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana
kwenye picha za hivi karibuni alizoposti
kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo
moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’
hiyo na nyingine hana.
Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo
walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda
kuwa alichokifanya siyo sawa.
“Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake,
alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo
hayo hayapo. Kitendo cha yeye kwenda Sauzi
na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau,
amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo
sawa, ” alisema shabiki wa Diamond
aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.
Diamond hakuweza kupatikana mara moja
kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake
huyo.
Source:Global Publishers