Tuesday, February 10, 2015

AUNTY EZEKIEL:NAAMINI KABISA HUYU MWANANGU ATAKUJA KUNIFUTA MACHOZI NA KUNIFARIJI KWA KUONDOKEWA NA WAZAZI WANGU WOTE

MKALI wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amefunguka kuwa pamoja na kupoteza wazazi wake miaka kadhaa nyuma pindi akiwa mdogo, anaamini mtoto atakayejifungua atamfuta machozi ya muda mrefu ya kuwapoteza wazazi wake.
Mkali wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Aunty alifunguka ishu hiyo kwa upole, ambapo alisema kifo cha wazazi wake kilimfanya kulelewa na bibi yake pamoja na shangazi.
“Kutokuwa na wazazi ni pigo kubwa kwangu, lakini hata hivyo naamini kwamba mwanangu atakuwa na furaha ambayo nilikuwa naipata kutoka kwa wazazi wangu, atakuwa ni zaidi ya rafiki au ndugu, ndiye atakayenifuta machozi ya kufiwa,” alisema Aunty.