Monday, November 3, 2014

HATARI SANA: JOHN TERRY WA CHELSEA AUSHANGAZA ULIMWENGU KWA HIKI ALICHOFANYA!


Nahodha wa Chelsea John Terry amekuwa na kawaida ya kukusanya vitambaa ambavyo amekuwa akivivaa kama nahodha wa Chelsea na timu ya taifa ya England kwa miaka yote ambayo amekuwa kiongozi wa timu hizo mbili ambazo amezichezea . 
Terry ambaye kwa sasa ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza cha Chelsea ambaye amekuwa na timu hiyo tangu akiwa na umri mdogo kwenye vikosi vya academy amepata mafanikio makubwa katika miaka yake yote akiwa na klabu hiyo . 

Terry kwenye moja ya mechi alizoiongoza England dhidi ya timu ya taifa ya Marekani . 
Terry amewahi kutwaa mataji karibu yote ikiwemo ubingwa wa ligi kuu ya England , Klabu bingwa ya Ulaya , Kombe la UEFA Europa , Kombe la FA na kombe la ligi . 

Kupitia ukirasa wake kwenye mtandao wa Instagram nahodha huyo wa The Blues aliuonyesha ulimwengu mkusanyiko wa vitambaa vya unahodha yaani Captain’s Armbands ambavyo amekuwa akivivaa katika maisha yake kama nahodha wa Chelsea na England na huenda akawa mchezaji ambaye ameiongoza klabu yake katika mechi nyingi kuliko wote  na hivi majuzi tu akiweka rekodi ya kuanza mchezo wake wa 500 akiwa na Chelsea .
 Terry akiwa na fulana inayoonyesha michezo 500 aliyoanza akiwa Chelsea.